• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga kithabiti kuenea kwa silaha za maangamizi

    (GMT+08:00) 2019-03-20 09:13:37

    Naibu balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao, amesema China inapinga kithabiti kuenea kwa silaha za maangamizi ya halaiki na njia za kufanya mashambulizi kwa silaha hizo.

    Balozi Wu alisema hayo alipohudhuria mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kutoeneza silaha za maangamizi. Amesema siku zote China inatekeleza wajibu wake wa kimataifa kwa makini katika kuzuia kuenea kwa silaha hizo, na kuchangia katika kutatua masuala makuu ya kuzuia kuenea kwa silaha hizo kwa njia ya kisiasa.

    Amesema China inapenda kuhimiza ushirikiano na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kushirikiana na nchi mbalimbali duniani katika kuboresha mfumo na usimamizi wa kimataifa wa kuzuia kuenea kwa silaha za maangamizi, ili kutoa mchango kwa pamoja katika kuletea amani na utulivu wa kudumu duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako