• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • VOLIBOLI: Pipeline na Prisons zaanza vizuri voliboli Cairo

    (GMT+08:00) 2019-03-20 09:37:53

    Klabu za Pipeline na Prisons za Kenya zimeanza vizuri kampeni zao za kusaka ubingwa kwenye mashindano ya voliboli ya wanawake ya Afrika jijini Cairo Misri.

    Pipeline inayofundishwa na Margaret Indakala imeipiga watoza ushuru wa Rwanda (RRA) kwa seti 3-0 za alama 25-19, 25-19 na 25-15.

    Mechi ya ufunguzi ya kundi C ilishuhudia FAP kutoka Cameroon ikibwaga Shooting kutoka Misri kwa seti 3-0 za 26-24, 25-14 na 25-22. Nao Prisons ilifungua mashindano hayo kwa kubwaga Asec Mimosa ya Ivory Coast kwa seti 3-0 za alama 25-12, 25-13 na 25-8 katika mechi ya Kundi D. Jumla ya timu 17 zinashiriki michuano hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako