• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: "Nitavua Glovu nikigonga miaka 40" asema Casillas

    (GMT+08:00) 2019-03-20 09:38:10

    Golikipa wa FC Porto Iker Casillas ameweza wazi mpango wake wa kuacha kusakata kabumbu atakapotimiza umri wa miaka 40. Nyota huyo aliyejiunga na FC Porto akitokea Real Madrid sasa anaumri wa miaka 37 ameshacheza mechi 34 kwenye ligi, klabu bingwa Ulaya (UEFA) na mashindano mengine nchini Ureno.

    Wiki hii kipa huyo anatarajiwa kuanguka saini kuongeza mkataba hadi mwaka 2022 ambapo amedai atastaafu soka. Casillas amejizolea sifa kedekede katika kipindi ambacho amekuwa kwenye ulingo wa soka baada ya kuongoza Uhispania kushinda kombe la dunia mwaka wa 2010 na pia kutwaa kombe la klabu bingwa barani Ulaya (UEFA) mara tatu akichezea Real Madrid ya Uhispania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako