• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping atoa makala kwenye chombo cha habari cha Italia

    (GMT+08:00) 2019-03-20 18:17:33

    Rais Xi Jinping wa China leo ametoa makala kwenye gazeti la II Corriere Della Sera la Italia, inayoitwa "mfano mzuri wa maingiliano kati ya Mashariki na Magharibi, urafiki kati ya China na Italia kufungua ukurasa mpya".

    Kwenye makala hiyo, rais Xi amesema, China na Italia ni wawakilishi wakubwa wa utamaduni wa Mashariki na Magharibi, na maingiliano ya kirafiki kati ya nchi hizo mbili yana historia ndefu. Tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi, China na Italia zinaaminiana, kushirikiana kwa karibu, na kuwa mfano wa kuigwa wa kunufaishana kati ya nchi zenye utaratibu tofauti wa kijamii, utamaduni tofauti na viwango tofauti vya maendeleo.

    Amesema, China inapenda kushirikiana na Italia kujenga "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kupanua maeneo ya ushirikiano, kuongeza maingiliano ya utamaduni, kuimarisha uratibu wa mambo ya kimataifa na ndani ya mashirika ya kimataifa, na pia kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kuhusu usimamizi wa dunia, kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, mageuzi ya Umoja wa Mataifa, mageuzi ya WTO, kulinda maslahi ya pamoja, kuhimiza hali yenye pande nyingi na biashara huria, na kulinda amani, utulivu na maendeleo kwa ustawi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako