• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya mambo ya nje ya China yazungumzia ziara ya rais Xi Jinping nchini Italia, Monaco na Ufaransa

    (GMT+08:00) 2019-03-20 18:23:08

    Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Chao leo ameeleza mambo atakayofanya rais Xi Jinping atakapokuwa ziarani katika nchi za Italia, Monaco na Ufaransa.

    Bw. Wang Chao amesema, akiwa nchini Italia, rais Xi atakutana na rais Sergio Mattarella wa Italia na waziri mkuu Bw. Giuseppe Contem, na kubalishana nao maoni kuhusu masuala ya kimataifa na kikanda yanayohusu pande hizo mbili. Rais Xi na Bw. Contem watashuhudia kusainiwa kwa nyaraka za ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta ya diplomasia, uchumi na biashara na utamaduni na makubaliano ya kibiashara katika sekta za miundo mbinu, mashine na fedha.

    Pia rais Xi atakutana na mfalme Albert II wa Monaco, na kujadiliana naye kuhusu ushirikiano kati ya China na Monaco katika sekta za siasa, uchumi, utamaduni wa binadamu na uhifadhi wa mazingira.

    Akiwa nchini Ufaransa, rais Xi atafanya mazungumzo na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, na watabadilishana maoni kuhusu uhusiano kati ya China na Ufaransa, kati ya China na Ulaya, na masuala ya kimataifa na kikanda yanayohusu pande hizo mbili.

    Bw. Wang Chao anaamini ziara ya Rais Xi itahimiza ushirikiano halisi kati ya China na Italia, Monaco na Ufaransa, kuweka nguvu mpya kwa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ulaya katika kipindi kipya, kufungua sekta mpya kwa ujenzi wa pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", kuwanufaisha watu wa China na Ulaya, na kutoa mchango mpya kwa amani na maendeleo ya dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako