• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania yawataka wafugaji kutumia mbegu zinazozalishwa na NAIC

  (GMT+08:00) 2019-03-20 18:39:53

  Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Elisante Ole Gabriel ameagiza halmashauri zote nchini humo kutoa elimu kwa wafugaji juu ya umuhimu wa kutumia mbegu bora zinazozalishwa kituo cha Taifa cha Uhimilishaji Mifugo kwa Njia ya chupa (NAIC) kilichoko Arumeru mkoani Arusha.

  Prof. Ole Gabriel alitoa agizo hilo katika ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, kutokana na mwamko mdogo wa kutumia mbegu hizo.

  Alisema ili kuendana na uchumi wa viwanda ni lazima wafugaji wabadilike na kutumia mbegu hizo ili kupata ng'ombe wenye nyama bora, maziwa, ngozi na kwato zitakazokidhi malighafi za viwanda.

  Katibu Mkuu huyo alisema kwa kipindi cha mwaka jana, walitoa mafunzo kwa wafugaji 58,000 kwa nchi nzima hali iliyosababisha kuzalisha ndama 10,000 pekee licha ya kituo hicho kuzalisha mbegu 60,000 kwa wiki.

  Pia alitumia fursa hiyo kuwataka wafugaji kuondokana na dhana potofu kwamba kutumia mbegu hizo ni kuharibu vizazi vya mifugo jambo ambalo si sahihi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako