• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyama vya siasa vya Afrika kusini vyaahidi mienendo mizuri kwenye uchaguzi

    (GMT+08:00) 2019-03-21 09:03:13

    Jumla ya vyama 49 vya siasa vya Afrika Kusini vimesaini ahadi ya kufuata sheria wakati wa kampeni na kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi utakaofanyika Mei 8. Ahadi hiyo imesainiwa mjini Johannesburg chini ya maelekezo ya Tume huru ya uchaguzi ya nchi hiyo.

    Mwenyekiti wa chama tawala cha ANC Bw. Cyril Ramaphosa amesema kupitia kusaini ahadi hiyo, chama chake kimeonesha dhamira ya kushirikiana na vyama vyote na wananchi wote wa Afrika Kusini katika kujenga demokrasia imara, ya kudumu na yenye msukumo.

    Afisa mkuu wa Tume ya uchaguzi ya Afrika Kusini Bw. Sly Mamabolo amesema hafla ya kusaini ahadi hiyo iliyofanyika Jumatano inaendana na Sheria ya uchaguzi, ambayo inavitaka vyama vya siasa vinavyoshiriki kwenye chaguzi za taifa na majimbo, viahidi hadharani kufuata sheria kwa makini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako