• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yatarajia kuunda serikali ya umoja mwezi Mei licha ya mashaka kutoka kwa upinzani

    (GMT+08:00) 2019-03-21 09:03:30

    Sudan Kusini imesema Serikali ya Umoja ya Mpito iliyosubiriwa kwa muda mrefu itaundwa mwezi Mei, licha ya mashaka kutoka vyama vya upinzani vinavyolalamikia kuchelewa kuunganishwa kwa jeshi na kuamua idadi ya majimbo na mipaka.

    Waziri wa habari wa Sudan Kusini Bw. Michael Lueth amesema serikali hiyo ya umoja itaundwa licha ya pande hasimu kuchelewa kukubaliana juu ya kuunganisha vikosi, kuamua idadi ya majimbo na mipaka.

    Naibu afisa habari wa chama kikuu cha upinzani SPLM-IO Bw. Manawa Gatkuoth, hivi karibuni alisema serikali ya umoja haiwezi kuundwa, kabla Kamisheni ya Mipaka ya Kimataifa haijaamua idadi ya majimbo na mipaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako