• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri Mkuu wa Tanzania azindua mradi wa maji uliojengwa na China kwa ajili ya watu elfu 50

    (GMT+08:00) 2019-03-21 09:15:16

    Waziri Mkuu wa Tanzania Bw. Kassim Majaliwa jana aliweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji katika eneo la Misungwi mkoani Mwanza, ili kuwanufaisha zaidi ya watu elfu 50.

    Mradi huo unaojengwa na kampuni ya China ni sehemu ya mradi mkubwa unaotekelezwa na serikali ya Tanzania chini ya mpango wa usambazaji maji katika ziwa Viktoria. Waziri Mkuu Majaliwa amesema mradi huo unajengwa kwa mkono wenye riba nafuu kutoka Benki ya uwekezaji ya China na Shirika la maendeleo la Ufaransa.

    Waziri Mkuu ameipongeza kampuni ya China itakayojenga mradi huo (CCECC) na kusema ni kampuni yenye uzoefu mkubwa kwenye ujenzi nchini China na duniani, na inaaminiwa na serikali ya Tanzania baada ya kujenga miradi mbalimali, ikiwa ni pamoja na daraja la ubungo, Dar es salaam.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako