• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tofauti kati ya China na Umoja wa Ulaya zinaweza kudhibitiwa

    (GMT+08:00) 2019-03-21 09:15:38

    Mkuu wa ujumbe wa China kwenye Umoja wa Ulaya Balozi Zhang Ming, amesema China na Umoja wa Ulaya zinajua namna ya kudhibiti na kuondoa tofauti kati yao ili kuendeleza uhusiano wenye afya kati yao.

    Balozi Zhang ametoa maoni hayo kwenye taasisi ya washauri bingwa ya Marafiki wa Ulaya, yenye makao yake mjini Brussels, na kusema anaamini kuwa uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya hauna mabadiliko makubwa, na unaweza kurekebishwa na kusonga mbele na kuendelea kusaidia kutuliza dunia.

    Balozi Zhang amesema hayo wakati wiki iliyopita Umoja wa Ulaya ulitangaza mpango wenye mapendekezo ya hatua 10 unaoitaja China kama ni mwezi wa ushirikiano, mshindani wa kiuchumi na hasimu wa kimfumo. Hata hivyo Balozi Zhang amesema licha ya kuwa China na Umoja wa Ulaya zina mifumo tofauti ya kisasa, hii haina maana kuwa wao ni mahasimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako