• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri Mkuu wa Uingereza atoa msimamo mkali kuhusu Brexit kwenye bunge la Uingereza

    (GMT+08:00) 2019-03-21 09:16:08

    Waziri Mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May amesema kuwa hatachelewesha Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya hadi baada ya mwezi juni, na kusema hakutakuwa na hali hiyo hata kama wabunge wakikataa makubaliano ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya Brexit.

    Bibi May amesema hayo baada ya mjadala mkali kwenye baraza la makabwela alipotangaza kuwa amemuomba mwenyekiti ya baraza la umoja wa Ulaya Bw Donald Tusk kuchelewesha Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya.

    Bibi May amewalaani wabunge wanaokataa makubaliano yake, na kusema kama wakiyakataa tena makubaliano yake, basi Uingereza itajitoa Umoja wa Ulaya bila kuwa na makubaliano yoyote.

    Hata hivyo wachambuzi wa mambo ya kisiasa wamesema Bibi May anakosea kuwakosoa wabunge, kwa kuwa atawategemea wabunge hao kupitisha makubaliano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako