• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kimbunga Idai chasababisha vifo vya watu zaidi ya 360 Kusini mwa Afrika

    (GMT+08:00) 2019-03-21 09:27:56

    Naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Farhan Haq jana amesema, Kimbunga cha Idai huenda ni moja ya majanga makubwa zaidi ya asili kulikumba eneo la Kusini mwa Afrika, ambacho kimesababisha vifo ya watu zaidi ya 360.

    Bw. Haq amesema hayo wakati akitoa ripoti kuhusu uharibifu uliosababishwa na kimbunga cha Idai nchini Malawi, Msumbuji na Zimbabwe.

    Bw. Haq amesema kuwa mkuu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Mark Lowcock, ametenga dola za kimarekani milioni 20 kutoka Mfuko wa Kukabiliana na Mambo ya Dharura wa Umoja wa Mataifa, ili kuunga mkono juhudi za serikali za Msumbiji, Zimbabwe na Malawi kutoa misaada kwa jamii zilizoathirika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako