• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe maalumu wa UN asema hali ya Libya imefikia kipindi muhimu

    (GMT+08:00) 2019-03-21 09:36:42

    Mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia suala la Libya Bw. Ghassan Salame, amesema hali ya Libya imefikia kipindi muhimu.

    Kwenye mkutano wa Baraza la usalama Bw. Salame amesema, wanafanya kazi ili kuzuia hali ya Libya isizidi kuwa mbaya, na wanajaribu kutatua mgogoro kwa mpango wa kisiasa, ambao unaweza kukomesha mgogoro nchini Libya.

    Bw. Salame amesema ingawa kulikuwa na matukio machache, lakini kitendo cha Januari 13 cha kuwasili kwa amani kwa vikosi vya Jenerali Khalifa Haftar mjini Sabha, kumeonekana kuwa ni maendeleo mazuri.

    Bw. Salame pia ni mkurugenzi wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Libya, ambayo imeunga mkono duru mbili zamazungumzo kati ya washauri wa waziri mkuu wa Libya Bw. Fayez Serraj and Jenerali Haftar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako