• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo ya vyombo vya habari kati ya China na Italia yajadili uhusiano na ushirikiano kati ya pande mbili

    (GMT+08:00) 2019-03-21 09:54:12

    Mazungumzo ya vyombo vya habari kati ya China na Italia yenye kaulimbiu ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja na ushirikiano wa vyombo vya habari kati ya China na Italia" yamefanyika kwenye Jumba la Makumbusho la Usanii ya karne ya 21 mjini Rome.

    Mazungumzo hayo ambayo ni shughuli muhimu inayofanyika kwa kufuata ziara ya rais Xi Jinping nchini Italia, yameandaliwa na vyombo vya habari vya China na Italia, na kuhudhuriwa na wajumbe wapatao 200 kutoka pande mbili.

    Akihutubia mazungumzo hayo, naibu mkuu wa Idara ya Uenezi ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Jiang Jianguo amesema, chini ya mfumo wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", Italia imekuwa ikifanya ushirikiano wenye ufanisi na China. Anaamini kuwa makubaliano muhimu yatakayofikiwa wakati wa ziara ya Rais Xi nchini Italia, yatazielekeza nchi hizo mbili kupata maendeleo kwenye ushirikiano kati yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako