• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Reli ya SGR ya Kenya yasafirisha abiria milioni 1.7 katika mwaka 2018

    (GMT+08:00) 2019-03-21 09:54:37

    Idara ya takwimu ya Kenya KNBS imesema, Reli ya SGR ya Kenya imesafirisha abiria milioni 1.7 katika mwaka 2018, idadi ambayo imezidi kwa mara mbili idadi ya abiria waliosafiri kwa huduma ya treni ya Madaraka Express tangu ilipoanzishwa katikati ya mwaka 2017, hadi mwisho wa mwaka 2017.

    Reli hiyo inachukua muda wa saa tano kusafiri kati ya miji ya Nairobi na Mombasa, kwa nauli ya dola za kimarekani 10 kwa daraja la pili, na dola 30 za kimarekani kwa daraja la kwanza, na watoto wanalipa nusu ya nauli.

    Reli hiyo ilisafirisha tani milioni 5.03 za mizigo katika mwaka 2018, na kuleta mapato ya dola za kimarekani laki 8.6.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako