• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NDONDI: Mwakinyo awasili Kenya tayari kuzichapa na Gonzalez

    (GMT+08:00) 2019-03-21 10:16:37

    Bondia nyota wa Tanzania, Hassan Mwakinyo, amewasili jijini Nairobi, Kenya tayari kwa pambano lake la kimataifa dhidi ya bondia kutoka Argentina, Eduardo Gonzalez, lililopangwa kufanyika Machi 23 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta.

    Mwakinyo alikuwa anafundishwa na kocha Muingereza, Tony Bellew akiwa kambini jijini Liverpool, England chini ya ufadhili wa Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya SportPesa.

    Bondia wa kike toka Kenya Fatuma Zarika, atapambana na Catherine Phiri wa Zambia katika pambamo la ubingwa wa dunia wa uzito wa Super Bantam weight wa baraza la ngumi za kulipwa duniani (WBC).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako