• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Zidane atafanikiwa kumvuta Mane, kukipiga Madrid?

    (GMT+08:00) 2019-03-21 10:17:52

    Klabu ya Read Madrid ya Uhispania sasa macho yake yamemgeukia mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane baada ya Zinedine Zidane kurejea katika dimba la Santiago Bernabeu.

    Baada ya kuonyesha kiwango bora msimu huu, mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal amekuwa lulu katika kikosi cha Liverpool akiwa ndiye mfungaji bora. Zidane ameanza kuisuka upya Real Madrid, anatakiwa kufanya kazi ya ziada ili kuweza kumsajili mchezaji huyo.

    Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ufaransa vimeeleza kuwa, Zidane amemuweka Mane kwenye orodha ya nyota anaowahitaji kwenye usajili wa majira ya kiangazi.

    Mwezi Novemba mwaka jana klabu ya Liverpool ilimuongeza mchezaji huyo mkataba ambao unamalizika mwaka 2023.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako