• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Makocha 50 bora wa muda wote watajwa

    (GMT+08:00) 2019-03-21 10:18:10

    Jarida la soka la Ufaransa ambalo hutoa tuzo ya Ballon D'Or limekuja na orodha ya makocha 50 bora wa soka duniani wa muda wote.

    Katika orodha hiyo, mfaransa mwenzao Arsene Wenger, anayeheshimiwa nchini Uingereza kwa kufanya mapinduzi makubwa ya soka nchini humo, amewekwa katika nafasi ya 32 kwenye orodha hiyo.

    Diego Simeone amekamata nafasi ya 31 huku Jose Mourinho akikamata nafasi ya 13. Nafasi ya kwanza imekwenda kwa Linus Michels alikuwa kocha wa Ajax ya Uholanzi na kuisaidia kushinda klabu bingwa Ulaya mara tatu mfululizo mwaka 1970/71, mwaka 1971/72 na mwaka 1972/73, pia aliisaidia klabu yake kushinda mataji 7 ya ligi na manne ya kombe la FA.

    Nafasi ya pili imeangukia kwa Sir Alex Ferguson gwiji wa Manchester United aliyeshinda taji la ubingwa wa ligi kuu mara 13, makombe 5 ya FA na ligi ya mabingwa mara 2.

    Jarida hilo wamepanga orodha hiyo kuzingatia mataji ambayo kocha mhusika ameshinda, ushawishi wake mchezoni yaani alileta kitu gani tofauti, haiba na hamasa aliyetengeneza na kusababisha vijana kuanza kufuatilia na kupenda soka na kushiriki.

    Pep Guardiola amekamata nafasi ya 5, Carlo Ancelotti amekamata nafasi ya 8, Fabio Capello ameshika nafasi ya 21 huku Zinedine Zidane amekamata nafasi ya 22, nafasi ya mwisho ya 50 imecjukuliwa na Jean-Claude Suaudeau.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako