• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiongozi wa juu wa Iran aitaka nchi hiyo kukabiliana na shinikizo la vikwazo vilivyowekwa na Marekani

    (GMT+08:00) 2019-03-21 16:51:12

    Kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ametoa wito wa uvumbuzi wa kiuchumi na kuboresha uzalishaji ili kukabiliana na shinikizo linalotokana na vikwazo vilivyowekwa na Marekani.

    Bw. Khamenei amesema hayo katika hafla ya kusherehekea Mwaka Mpya wa Iran ambao unaanza leo. Amesema ingawa adui wa nchi hiyo walitega mitego mingi, lakini uvumilivu wa vijana pamoja na ushupavu na busara ya taifa hilo vilishinda hila hizo.

    Wakati huohuo, Khamenei amekiri kuwepo kwa hali mbaya kiuchumi, ikiwemo ugumu wa maisha ya watu, na kutaka uongozi wa nchi hiyo kukabiliana na wasiwasi wa kiuchumi wa wananchi wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako