• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Naibu waziri mkuu wa China ashiriki kwenye mkutano wa pili wa ushirikiano wa kusini na kusini

    (GMT+08:00) 2019-03-21 16:54:01

    Naibu waziri mkuu wa China Bw. Hu Chunhua ameshiriki kwenye mkutano wa pili wa Umoja wa Mataifa wa ushirikiano wa kusini na kusini uliofanyika mjini Buenos Aires, Argentina.

    Bw. Hu amesema, China inaendelea kuunga mkono mfumo wa pande mbalimbali wa Umoja wa Mataifa na kuendelea kulinda kanuni za ushirikiano wa kusini na kusini za kuheshimu mamlaka, kunufaishana na kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine. Anatarajia mkutano huo utafikia makubaliano na kutoa mchango kwenye utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030.

    Bw. Hu pia amesema, China itaendelea kuwajibika na majukumu ya kimataifa kwa kufuata uwezo wake na kushirikiana na nchi mbalimbali kujenga kwa pamoja jumuiya yenye hatma ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako