• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima wa korosho Mtwara walalama kuhusu ucheleweshaji wa malipo ya korosho

    (GMT+08:00) 2019-03-21 19:58:51

    Wakulima wa korosho mkoani Mtwara, wameliomba Bunge kuingilia kati ucheleweshwaji wa malipo yao kwa kuishinikiza serikali kutekeleza kwa vitendo ahadi inazozitoa kwa kile walichokidai kuwa wamechoshwa na matamko yanayokosa utekelezaji.

    Kwa nyakati tofauti, wakizungumza na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji katika wilaya za Tandahimba na Newala mkoani hapo jana, wakulima hao walisema licha ya serikali kutoa maagizo kwa watendaji kuwalipa wakulima fedha zao, utekelezaji wake umekuwa wa polepole.

    Walisema iwapo Bunge litaingilia kati kwa kuisimamia serikali kuhakikisha wakulima wa korosho wanalipwa fedha zao kwa wakati, itasaidia kuwatatulia shida walizo nazo zikiwamo madeni yanayotokana na vibarua na maandalizi ya msimu ujao.

    Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Namkulya Suleiman Namkulya, alisema mbali na wakulima kutolipwa fedha zao pia kukosekana kwa ushuru kumeiathiri halmashauri hiyo kwa asilimia 100.

    Alisema asiliamia 95 ya mapato yao ya ndani yanategemea korosho, asilimia tano inategemea mnyororo wa thamani ya korosho, hivyo kwa asilimia 100 wanategemea korosho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako