• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China awasili Italia kwa ziara rasmi

    (GMT+08:00) 2019-03-22 09:16:42

    Rais Xi Jinping wa China jana aliwasili mjini Rome kuanza ziara rasmi nchini Italia.

    Rais Xi na mke wake Bibi Peng Liyuan waliwasili jana jioni katika uwanja wa ndege wa Fiumicino mjini Rome, ambako alikaribishwa na waziri wa kilimo na utalii wa Italia na maofisa wengine waandamizi wa serikali ya nchi hiyo.

    Rais Xi amesema uhusiano kati ya China na Italia umepitia majaribu yanayotokana na wakati, na mabadiliko ya mazingira ya kimataifa tangu ulipoanzishwa miaka 49 iliyopita. Lakini nchi hizo mbili zimeendelea kukuza urafiki na ushirikiano kwenye msingi wa kuheshimiana, kuaminiana na kunufaishana, na kuweka mfano wa kuigwa wa kuendeleza uhusiano kati ya nchi zenye mifumo tofauti, tamaduni tofauti na viwango tofauti vya maendeleo.

    Rais Xi amesema anatarajia kukutana na mwenzake wa Italia Bw. Sergio Mattarella, waziri mkuu Bw. Giuseppe Conte na viongozi wengine wa Italia, ili kuweka mipango kwa pamoja kwa ajili ya maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili katika siku zijazo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako