• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China aanza ziara barani Ulaya

    (GMT+08:00) 2019-03-22 09:17:21

    Rais Xi Jinping wa China jana jioni aliwasili katika uwanja wa ndege wa Fiumicino mjini Rome, na kuanza ziara rasmi nchini Italia, ambayo ni kituo cha kwanza cha safari yake katika nchi tatu za Ulaya.

    Kwenye taarifa aliyoitoa kwenye uwanja wa ndege, rais Xi amezungumzia historia ya uhusiano kati ya China na Italia, maendeleo ya uhusiano huo tangu ulipoanzishwa, na mafanikio yaliyopatikana kwenye ushirikiano wa nchi hizo mbili.

    Rais Xi amesema anatarajia kukutana na mwenzake wa Italia Bw. Sergio Mattarella, waziri mkuu Bw. Giuseppe Conte na viongozi wengine wa Italia, ili kuweka mipango kwa pamoja kwa ajili ya maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili katika siku zijazo.

    Huu ni mwaka wa 15 tangu China na Italia zianzishe uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote. Italia ni kituo cha kwanza cha ziara ya rais Xi katika nchi tatu za Ulaya, ambayo pia ni ziara yake ya kwanza katika nchi za nje kwa mwaka huu. Wachambuzi wanaona kuwa Rais Xi kuchagua kutembelea nchi tatu za Ulaya katika ziara yake ya kwanza kwa mwaka huu, kumeonesha kuwa China inatilia maanani kukuza uhusiano kati yake na Ulaya.

    Rais Xi Jinping siku zote anatilia maanani maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ulaya. Miezi mitatu iliyopita, alifanya ziara nchini Hispania na Ureno; Miaka mitano iliyopita, alifanya ziara yake ya kwanza barani Ulaya tangu alipochaguliwa kuwa rais wa China, ambapo amekuwa rais wa kwanza wa China kutembelea makao makuu ya Umoja wa Ulaya tangu pande hizo mbili zilipoanzisha uhusiano wa kibalozi, kwa mara ya kwanza alitoa pendekezo la kuendeleza uhusiano kati ya China na Ulaya kwenye nyanja nne za amani, maendeleo, mageuzi na ustaarabu, na pia ni kwa mara ya kwanza alifafanua msimamo wa China kuhusu usalama wa nyuklia.

    Wachambuzi wanaona kujenga kwa pamoja "Ukanda mmoja, Njia moja" kunaweza kuwa moja ya ajenda muhimu kwenye ziara hiyo. Naye waziri mkuu wa Italia Bw. Giuseppe Conte hivi karibuni amesema anatarajia kushuhudia kwa pamoja na rais Xi jinping kusainiwa kwa makubaliano ya ushirikiano kati ya China na Italia kuhusu "Ukanda Mmoja, Njia moja". Amesema ushirikiano huo utarithi na kuenzi njia ya hariri ya zama za Marco Polo, na kusukuma mbele uhusiano kati ya Italia na China ufikie ngazi mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako