• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Afrika Kusini yasema iko makini katika kupambana na msukosuko wa nishati

    (GMT+08:00) 2019-03-22 09:28:02

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema serikali iko makini katika kukabiliana na tatizo la kukatika kwa umeme linaloiathiri nchi hiyo kwa sasa.

    Akiongea mjini Sharpeville kwenye maadhimisho ya siku ya haki za binadamu, Rais Ramaphosa amesema tatizo hilo limekuwa ni msukosuko mkubwa wa nishati unaoleta madhara kwa maisha na uchumi wa nchi, na kwamba kurudisha umeme wa kuaminika, na kuwa na mtindo wa umeme wa gharama nafuu, ni jambo la kipaumbele kwa serikali ya Afrika Kusini.

    Katika miaka ya hivi karibuni Afrika Kusini imekuwa inakabiliwa na tatizo kubwa la kukatika kwa umeme, na imefikia wakati kuna mgao wa umeme kwa muda wa wiki. Kampuni ya Goldman Sachs imesema kama hali ya sasa itaendelea, itaondoa asilimia 0.9 ya ongezeko la uchumi wa Afrika Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako