• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri Mkuu wa China asisitiza utekelezaji wa upunguzaji mkubwa wa kodi

    (GMT+08:00) 2019-03-22 09:28:41

    Waziri Mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesisitiza kuhusu utekelezaji mkubwa wa upunguzaji kodi ili kuhimiza uhai kwenye makampuni, hali ambayo itasaidia uchumi uendelee kwa kiwango cha wastani na kuhimiza maendeleo ya kiwango cha juu.

    Akiongea kwenye kongamano wakati wa ziara ya ukaguzi kwenye wizara ya fedha na mamlaka ya Kodi, Waziri Mkuu Li amesema kupunguza kodi na ada mbalimbali kutaleta manufaa kwa nchi katika muda mfupi na muda mrefu ujao, kwa kuwa sio tu kutapunguza mzigo wa kodi na kutuliza suala la ukosefu wa ajira, lakini pia utaongeza mgawanyo wa uchumi na mapato na kuhimiza matumizi endelevu.

    Waziri mkuu amesema makampuni yote yataona kupungua kwa kodi, na sio kuongezeka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako