• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe yatangaza siku mbili za maombolezo baada ya kimbunga cha Idai kusababisha vifo 139

    (GMT+08:00) 2019-03-22 09:29:02

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ametangaza siku mbili za maombolezo ya taifa kufuatia vifo vya watu 139 vilivyotokana na kimbunga cha Idai, na kusababisha madhara makubwa kwenye maeneo ya kusini na mashariki mwa nchi hiyo.

    Akilihutubia taifa jana, Rais Mnangagwa ametangaza leo na kesho kuwa siku za taifa za maombolezo, na pia amezishukuru serikali za nje, mashirika na watu walionyesha huruma kwa Zimbabwe wakati wa msiba mkubwa wa taifa na wa mahitaji makubwa.

    Kimbunga hicho ambacho kilitokea nchi jirani ya Msumbiji, pia kimesababisha maelfu ya watu kukosa makazi, baada ya nyumba zao kubomolewa kwa mvua.

    Serikali pia imesema watu 150 hawajulikani walipo kutokana na kimbunga hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako