• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China ataka juhudi zote zitumike katika uokoaji kufuatia mlipuko uliotokea kwenye eneo la viwanda

    (GMT+08:00) 2019-03-22 18:44:45

    Rais Xi Jinping wa China ametaka juhudi zote zitumike katika kazi ya uokoaji baada ya mlipuko uliotokea kwenye eneo la viwanda mkoani Jiangsu kusababisha vifo na majeruhi ya watu kadhaa.

    Rais Xi ambaye yuko ziarani nje ya nchi, ameagiza juhudi zote zitumike kuwaokoa wale waliokwama, majeruhi wapatiwe matibabu, na majukumu yote kutekelezwa kikamilifu ili kudumisha utulivu wa jamii.

    Wakati huohuo, Baraza la Serikali la China limeunda timu ya uchunguzi wa mlipuko huo itakayoongozwa na naibu waziri wa usimamizi wa majanga ya dharura Bw. Huang Ming.

    Watu 47 wamefariki na wengine 90 kujeruhiwa vibaya baada ya mlipuko kutokea kwenye eneo la viwanda vya kemikali mjini Yancheng, Jiangsu, mashariki mwa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako