• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Marekani atambua mamlaka ya Israel katika eneo la milima ya Golan

    (GMT+08:00) 2019-03-22 19:50:33

    Rais Donald Trump wa Marekani amesema, nchi yake inapaswa kutambua mamlaka ya Israel katika eneo la milima ya Golan.

    Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameishukuru Marekani kwa kuunga mkono masuala ya usalama wa haki ya kujilinda ya Israel.

    Lakini katibu mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Bw. Ahmad Abdoul Gheit ametoa taarifa akisisitiza kuwa, kwa mujibu wa sheria ya kimataifa na maazimio ya Umoja wa Mataifa, eneo hilo ni sehemu ya Syria, na jumuiya hiyo inunga mkono kikamilifu mamlaka ya Syria katika eneo hilo.

    Habari zinasema, mpaka sasa, ikulu ya Marekani bado haijaonyesha msimamo rasmi kuhusu kauli ya rais Trump.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako