• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Marekani kuchukua hatua halisi za kuendeleza uhusiano wa kijeshi kati yake na China

    (GMT+08:00) 2019-03-22 19:55:52

    Msemaji wa wizara ya ulinzi ya China Bw. Wu Qian ameitaka Marekani iache mawazo ya vita ya baridi, na kuchukua hatua halisi za kuendeleza uhusiano kati yake na China na uhusiano wa kijeshi kati ya nchi hizo mbili.

    Hivi karibuni, kaimu waziri wa ulinzi wa Marekani Patrick Shanahan na mwenyekiti wa kamati ya maofisa waandamizi ya jeshi la Marekani Joseph Dunford walilalamikia "tishio la China" kwenye mkutano wa baraza la juu kuhusu bajeti ya kijeshi. Bw. Wu amesema China inapinga kithabiti kauli hiyo ambayo itadhuru maendeleo ya uhusiano kati ya Marekani na China na uhusiano wa kijeshi kati yao.

    Bw. Wu amesema China inashikilia njia ya amani, na sera ya kujilinda, na siku zote China ni mjenzi wa amani ya dunia na mlinzi wa utaratibu wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako