• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KCB yaungana na benki ya Morocco kufanya biashara kimataifa

    (GMT+08:00) 2019-03-22 20:06:16
    Benki ya Kenya Commercial imetia saini mkataba na Benki ya Attijariwafa ya Morocco kwa lengo la kuimarisha biashara ya kimataifa.

    Mkataba huo uliotiwa sahihi Casablanca, Morocco, unatarajiwa kuimarisha ushirika katika utoaji wa huduma bora zaidi katika benki, huduma za fedha za biashara eneo la Africa Mashariki na Kaskazini Afrika.

    Ushirikiano kati ya benki hizo utaendeshwa kupitia kwa mpango wa dijitali na simu za mkononi.

    Afisa mkuu wa operesheni wa KCB, Samuel Makome amesema hatua hiyo itapelekea kuanzishwa kwa huduma za benki kwa niaba ya nyingine kwa lengo la kuwezesha operesheni za benki hizo na uhusiano wa kibiashara.

    Mkutano huo ni sehemu ya misheni ya Attijariwafa ya kukuza uwekezaji kati ya benki za Afrika, biashara na ushirikiano.

    Hii itatoa nafasi mpya sokoni kwa wateja hasa mashirika ya humu nchini, biashara ndogo na miradi ya kina mama.

    Benki hizo pia zitashirikiana kuhusiana na utoaji wa mafunzo na ajira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako