• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa UN Nairobi watoa wito wa kutumiwa kwa fursa zilizopo kukabiliana na umaskini

    (GMT+08:00) 2019-03-22 20:06:35

    Mawaziri wa mazingira kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa (UN) wamebaliana kutumia fursa zilizopo kukabiliana na umasikini uliopo barani Afrika. Hii ni baada ya wiki mbili za majadiliano na kutafuta suluhu kwa changamoto zilizopo,

    Licha ya kupambana na umasikini, mawaziri hao wamekubaliana kubadili namna ya uzalishaji na matumizi ya rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya wananchi. Katika kufanikisha hilo, matumizi ya teknolojia yatapewa kipaumbele zaidi.

    Wakati mawaziri hao wakitoa kipaumbele kwa ubunifu unaoonyeshwa na wajasiriamali wadogo, takriban watu 5,000 waliohudhuria mkutano wa nne wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) jijini Nairobi walivutika kutembelea banda la Newton Owino, mjasiriamali anayezalisha bidhaa kwa kutumia ngozi ya samaki.

    Owino anatambulika na UNEP kutokana na bidhaa zake zinazotokana na uchafu ulioachwa baada ya kuondoa minofu ya sangara wanaovuliwa Ziwa Viktoria.

    Owino hutengeneza mikoba, mikanda, ngoma na hata nguo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako