• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chama tawala cha Afrika Kusini chasema kitapambana na ufisadi wakati uchunguzi ukiendelea

    (GMT+08:00) 2019-03-23 17:42:34

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema chama tawala cha Afrika Kusini ANC kimedhamiria kuondoa ufisadi ambao umedhoofisha imani yake kwa umma, na kitafanya kila linalowezekana kurekebisha makosa.

    Akiongea kwenye mkutano wa kampeni mjini Cape Town, Rais Ramaphosa amekiri kuwa kashfa za ufisadi zimekiathiri chama cha ANC, na zinaweza kuwakatisha tamaa wapiga kura kukipigia kura kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Mei 8.

    Rais Ramaphosa amesema ni lazima chama cha ANC kiseme ukweli kuhusu kashfa ya ufisadi ya "kutekwa kwa dola", akimaanisha ushirikiano kati ya familia ya Gupta na maofisa waandamizi wa serikali ya Afrika Kusini kwenye wizi wa fedha za umma.

    Kwa mujibu wa kura za maoni asilimia 54.7 ya watu waliohojiwa watakipigia kura chama cha ANC, ikiwa imepungua kutoka asilimia 62.1 za mwaka 2014.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako