• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tajiri mkubwa wa Kenya akamatwa na dawa za kulevya zenye thamani ya dola elfu 15

    (GMT+08:00) 2019-03-23 17:43:06

    Tajiri mkubwa wa Kenya Abdulmajid Timami amekamatwa Ijumaa huko Mombasa na maofisa wa idara ya uchunguzi wa makosa ya jinai akiwa na dawa za kulevya aina ya Heroine, zenye thamani ya shilingi milioni 1.5 za Kenya, sawa na dola elfu 15 za Marekani.

    Ofisa mmoja wa polisi amesema mtuhumiwa huyo anayemiliki malori ya kusafirisha mizigo, amekuwa akijihusisha na biashara ya dawa za kulevya kwa karibu muongo mmoja, lakini sasa yuko mbaroni na atafikishwa mahakamani jumatatu.

    Kwa mujibu wa mamlaka husika, kuna soko kubwa la mihadarati huko Mombasa nchini Kenya, ambako wafanyabiashara wakubwa, wanasiasa na wana usalama wanafanya kazi. Mji huo pia ni lango la kusafirisha mihadarati na bidhaa za wanyama zilizopigwa marufuku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako