• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa China na Italia wafanya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2019-03-23 18:33:45

    Rais Xi Jinping wa China ameanza ziara yake nchini Italia na kufanya mazungumzo na mwenyeji Bw. Sergio Mattarella.

    Rais Xi amesema China na Italia ni nchi zenye ustaarabu wa kale, na uhusiano kati ya nchi mbili una historia ndefu. Pande zote mbili zinapaswa kudumisha mawasiliano ya kijamii na kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kwenye sekta za utamaduni, elimu, filamu na vyombo vya habari. Pia zinatakiwa kuimarisha kuunganisha mikakati, kutafuta fursa zaidi kwenye sekta za ujenzi wa miundombinu, shughuli za uchukuzi bandarini, usafiri wa meli na nyinginezo, kuanzisha miradi ya ushirikiano wa kiutendaji na kupanua mawasiliano ya kijamii kwa kufuata pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Kwa upande wa Italia, rais Mattarella amesema nchi zote mbili zinatilia maanani kudumisha ustaarabu, na wananchi wa nchi mbili wana busara za kutosha katika kukabiliana na changamoto wanazokabiliana nazo hivi leo. Amesema Italia inaunga mkono pendekezo la "Ukanda Mmoja Njia Moja", ambalo linaweza kusaidia maendeleo ya pamoja na kuunganishana mabara ya Ulaya na Asia.

    Wakati huo huo, rais Xi Jinping jana alikutana na spika wa baraza la chini la bunge la Italia Bw. Roberto Fico mjini Rome. Rais Xi alisisitiza kuwa ushirikiano na mawasiliano kati ya idara za utungaji wa sheria ni moja ya njia muhimu za kuzidisha maelewano na kuimarisha urafiki kati ya wananchi wa nchi mbili. Amesema China inaziunga mkono idara hizo katika kubadilishana uzoefu juu ya mambo ya utungaji wa sheria na utawala wa nchi. Pia amesema China inapenda kushirikiana na nchi za Umoja wa Ulaya kuimarisha ushirikiano kati ya pande mbili.

    Bw Fico amesema China ni mwenzi muhimu wa ushirikiano. Baraza la chini la bunge la Italia linadhamira kuhimiza mawasiliano na ushirikiano na China kwenye sekta za uchumi, biashara na utamaduni chini ya mfumo wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kuimarisha mawasiliano na uratibu na China, juu ya mabadiliko ya hali ya hewa na Ajenda ya maendeleo endelevu ya kuelekea mwaka 2030.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako