• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi mpya wa China nchini Kenya asema uhusiano kati ya China na Kenya utaimarika zaidi

    (GMT+08:00) 2019-03-23 18:34:37
    Balozi mpya wa China nchini Kenya Bw. Wu Peng amewasili Kenya jana na kupokewa na ofisa wa wizara ya mambo ya nje na biashara ya kimataifa anayeshughulikia na mambo ya Asia na Australia Bw. Christopher Chika.

    Akihojiwa na vyombo vya habari, Balozi Wu alisema katika miaka ya hivi karibuni, China na Kenya zimekuwa zikishirikiana na kuungana mkono katika masuala ya kikanda na ya kimataifa yenye maslahi kuu kwa kila upande, ambao ni uthibitisho muhimu wa uhusiano imara kati ya nchi hizo mbili. Mafanikio ya utekelezaji wa miradi kadhaa muhimu ukiwemo mradi wa Reli ya SGR yameanza kuleta faida, na wananchi wa nchi hizo mbili wanafurahia kuimarika kwa uhusiano huo.

    Imefahamika kuwa Kenya itapeleka ujumbe wa ngazi ya juu kuhudhuria mkutano wa pili wa kilele wa Baraza la ushirikiano la Ukanda Mmoja Njia Moja utakaofanyika mwezi Aprili mjini Beijing, China.

    Balozi Wu aliongeza kuwa, pendekezo la Ukanda Mmoja Njia Moja lilitolewa na China, lakini linawashirikisha walimwengu wote. Hivyo hakika China inaheshimu maoni Wakenya katika utekelezaji wa miradi inayohusisha Kenya, pia China inatafakari ipasavyo miradi inayopendekezwa na Kenya ili iwe endeleva na kuwa na faida nzuri kwa Wakenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako