• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Italia yajiunga na familia ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja"

    (GMT+08:00) 2019-03-23 21:02:35

    Serikali za China na Italia leo zimesaini Makubaliano kuhusu kuhimiza kwa pamoja utekelezaji wa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Zeozi hilo lililofanyika mjini Rome, Italia, lilishuhudiwa na rais Xi Jinping wa China na waziri mkuu wa Italia Bw Giuseppe Conte. Italia imekuwa nchi ya kwanza kwenye kundi la nchi saba za magharibi kusaini makubaliano kama hayo na China.

    Taarifa ya pamoja iliyotolewa na China na Italia inasema, pande zote mbili zimetambua uwezekano mkubwa wa pendekezo la "Ukanda Mmoja Njia Moja" juu ya kuhimiza kuungana kwa miundombinu, na zinapenda kuimarisha kuunganisha pendekezo hilo na mtandao wa usafiri barani Ulaya, kuhimiza ushirikiano kwenye sekta za bandari, shughuli za uchukuzi na usafiri wa baharini.

    Hadi sasa, idadi ya nchi na mashirika ya kimataifa yanayosaini makubaliano na China kuhusu utekelezaji wa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" imezidi 150, tangu rais Xi Jinping atoe pendekezo hilo mwaka 2013. Hivi sasa, China ni mwenzi mkubwa zaidi wa biashara kwa Italia barani Asia, na Italia ni mwenzi wa tano wa biashara na nchi ya tano kati ya nchi za Umoja wa Ulaya kwenye uwekezaji wa moja kwa moja nchini China. Kusainiwa kwa makubalinao hayo kunazipatia nchi hizo mbili fursa kubwa zaidi ya ushirikiano wa kiutendaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako