• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China afanya mazungumzo na waziri mkuu wa Italia

    (GMT+08:00) 2019-03-24 17:41:25

    Rais Xi Jinping wa China jana alifanya mazungumzo na waziri mkuu wa Italia Bw Giuseppe Conte mjini Rome.

    Rais Xi amesema China na Italia ni wenzi muhimu wa kimkakati, na China inapenda kushirikiana na Italia katika kuzidisha uhusiano kati ya pande mbili. Amesema nchi zote mbili zinapaswa kuunganisha pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na mipango ya Italia ya "ujenzi wa bandari wa kaskazini" na "kuwekeza nchini Italia", kupata mafanikio mapema kwenye sekta za teknolojia, ujenzi wa miundombinu, usafiri, mazingira na nishati, kuhimiza kwa pamoja ushirikiano wa masoko ya upande wa tatu, ikiwa ni pamoja na sekta za nishati, fedha, jamii na michezo, kuimarisha mawasiliano juu ya masuala makuu ya kiamataifa na kulinda utaratibu wa dunia yenye ncha nyingi. Pia amesema China inakaribisha nchi za nje kuwekeza nchini China, na kuitaka Italia iendelee kuweka mazingira mazuri ya kibiashara kwa wawekezaji wa China.

    Waziri mkuu Bw Conte amesema Italia inatilia maanani uhusiano na China, inapenda kuzidisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote na China, na kupanua ushirikiano kwenye sekta za uchumi, biashara, uwekezaji, nishati, kilimo, utamaduni, utalii na usafiri wa anga. Pia amesema Italia inakaribisha makampuni ya China kuwekeza nchini humo, kuunga mkono kithabiti utaratibu wa dunia yenye ncha nyingi na biashara huria, na kudumisha mawasiliano na uratibu na China ili kuhimiza uhusiano kati ya Ulaya na China uendelee vizuri kwa utulivu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako