• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa UNICEF atoa mwito wa kuwasaidia watoto walioathiriwa na kimbunga cha Idai

    (GMT+08:00) 2019-03-24 17:42:57

    Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa mataifa UNICEF Bibi Henrietta Fore, ametoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kutoa msaada kwa watoto walioathiriwa na kimbunga cha Idai.

    Wiki moja baada ya kimbunga cha Idai kuukumba mji wa bandari wa Beira, Msumbiji sasa madhara ya kimbunga hicho yanaonekana zaidi. Bibi Fore amesema sasa wanakimbizana na muda ili kusaidia kuwalinda watoto kwenye maeneo yaliyoathiriwa.

    Taarifa za awali zinaonyesha kuwa zaidi ya watu milioni 1.8, ikiwa ni pamoja na watoto laki 9, wameathiriwa na kimbunga hicho.

    Bibi Fore ameonya kuwa wakati operesheni za utafutaji na uokoaji zinaendelea, ni muhimu kuchukua hatua kuzuia magonjwa yanayoenea kwa njia ya maji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako