• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ziara ya rais Xi Jinping yatarajiwa kuchangia ukuaji wa uhusiano wa China na Monaco

    (GMT+08:00) 2019-03-24 18:12:28

    Wakati nchi ya Ulaya, Monaco inaposubiri kwa hamu ziara ya rais Xi Jinping wa China, ziara hiyo hakika itachangia ukuaji wa uhusiano wa nchi hizo mbili, na kuweka mfano mzuri wa usawa na urafiki kati ya nchi kubwa na ndogo.

    Kutokana na mwaliko wa mfalme wa Monaco Prince Albert II, rais wa China Xi Jinping ataanza ziara yake ya kwanza katika nchi hiyo yenye eneo la kilomita 2.02 za mraba, ambayo ni nchi ndogo ya pili duniani. Monaco ni kituo cha pili katika ziara ya rais Xi, ambaye sasa yupo nchini Italia.

    Balozi Zhai Juan amesema, uhusiano kati ya nchi hizo mbili unaendelea mzuri, na Prince Albert II amewahi kufanya ziara nchini China mara kumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako