• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China afanya mazungumzo na Prince Albert II wa Monaco

    (GMT+08:00) 2019-03-25 09:23:53

    Rais Xi Jinping wa China jana alifanya mazungumzo na Prince Albert II wa Monaco. Rais Xi Jinping amesema tangu miaka 20 iliyopita China na Monaco zianzishe uhusiano wa kibalozi, zimekuwa na urafiki wa dhati, na kutendeana kwa usawa. Amesema pande hizo mbili zinapaswa kushikilia ushirikiano ulio wazi, na kuzidisha hali ya kunufaishana. Amesema China inakaribisha Monaco kushiriki kwenye ushirikiano wa kimataifa wa ujenzi wa "Ukanda MMoja, Njia Moja".

    Prince Albert II amemkaribisha rais Xi na kusema uhusiano kati ya Monaco na China umeendelezwa vizuri. Amesema Monaco inapenda kupanua ushirikiano na China katika sekta za sayansi na teknolojia, uvumbuzi, uhifadhi wa mazingira, uhifadhi wa wanyamapori, nishati endelevu na kadhalika.

    Kabla ya mazungumzo yao Prince Albert II alimwandalia rais Xi hafla ya kumkaribisha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako