Burundi imefuzu kucheza michuano hiyo kwa mara ya kwanza baada ya mchezo wao kumalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1. DRC nao wamefanikiwa kufuzu baada ya kuipiga Liberia goli 1-0 katika uwanja wa Tata Raphael mjini Kinshasa. Kimbembe kilikuwa jana kwa Tanzania, kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39 timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars wameunagana na wenzao wa Afrika Mashariki kufuzu michuano hiyo baada ya kuichapa Uganda Cranes mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
kwa mara ya kwanza Afrika Mashariki inaingiza mataifa matano (Uganda, Kenya, Tanzania, Burundi na DRC) katika fainali za AFCON .
Mataifa mengine 19 ambayo tayari yamefuzu ni Angola, Madagascar, Tunisia, Misri, Senegal, Nigeria, Mali, Morocco, Algeria, Ivory Coast, Mauritania, Guinea, Ghana, Guinea Bissau, Namibia na Cameroon
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |