Kundi B, Luxembourg imeifunga Lithuania goli 2-1, huku Ureno ikitoka sare na Ukraine. Kundi D, Uswisi imeibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Georgia, na kundi H, Uturuki imeifunga Albania bao 2-0, Iceland wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Andorra na Ufaransa ikiichakaza Moldova mabao 4-1.
Michuano mingine imepigwa jana na usiku wa kuamkia leo, Kundi D Ireland imeifunga Gibraltar goli 1-0, huku Group E, Wales imetoka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Slovakia. Matokeo ya kundi F, Malta wameifunga Kisiwa cha Faroe goli 2-1, nayo Sweden wakiibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Romania, na Uhispania imeshinda 2-1 dhidi ya Norway.
Katika kundi I, Kazakhstan imekubali kichapo cha 4-0 toka kwa Urusi, na kundi H, Italia imeipiga Finland 2-0, Greece wameipiga Liechtenstein 2-0.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |