• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti yasema uchumi wa Ukanda wa Gaza umeingia katika hali mbaya zaidi katika miaka miongo kadhaa iliyopita

    (GMT+08:00) 2019-03-25 19:05:52

    Chama cha viwanda na biashara cha Ukanda wa Gaza hivi karibuni kimetoa ripoti ikisema, uchumi, maisha ya watu na hali ya kibinadamu katika Ukanda huo imeingia katika hali mbaya zaidi katika miaka miongo kadhaa iliyopita.

    Ripoti hiyo imesema, kutokana na ongezeko la vikwazo dhidi ya Ukanda wa Gaza, pande mbalimbali za ndani za Palestina zimetengwa, migogoro mbalimbali imeongezeka. Ripoti hiyo imesema, Israel kuendelea kuzuia vifaa vya ujenzi kuingia katika Ukanda wa Gaza ni chanzo kikuu cha kusababisha uchumi wa kanda hiyo kushuka.

    Ripoti hiyo imeonesha kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira katika Ukanda huo kimefikia asilimia 52, na kiwango cha umaskini kimefikia asilimia 53, huku asilimia 68 ya familia zikikabiliwa na uhaba wa chakula, na watu zaidi ya milioni 1 wanaishi kwa kutegemea msaada wa Umoja wa Mataifa. Mbali na hayo, idadi ya malori yanayoruhusiwa kupeleka mizigo katika kanda hiyo imepungua kutoka 750 kwa siku hadi 350.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako