• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soko la hisa la Nairobi (NSE) limeandikisha kupungua faida kwa asilimia 11.8 hadi Sh190.7mn kwa mwaka ulioisha Disemba 2018,kutokana na gharama kubwa

    (GMT+08:00) 2019-03-25 19:18:56
    Soko la hisa la Nairobi (NSE) limeandikisha kupungua faida kwa asilimia 11.8 hadi Sh190.7mn kwa mwaka ulioisha Disemba 2018,kutokana na gharama kubwa.

    Kupungua huko kumetokea licha ya mapato ya jumla kuongezeka kwa asilimia 4 hadi Sh782 milioni, hasa yaliyochangiwa na ongezeko la asilimia 2 katika usawa wa mauzo hadi Sh351 bilioni na asilimia 29 katika mauzo ya dhamana hadi Sh1.13 trillion.

    Katika kipindi hicho,gharama za utawala ziliongezeka kwa asilimia 13 kutoka Sh496 milioni katika mwaka 2017 hadi Sh560 milioni.

    Uongozi wa soko la hisa la Nairobi walisema hilo limesababishwa na upitiaji na mabadiliko ya mishahara na upungufu katika thamani ya jengo la NSE.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako