• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sekta ya Uchukuzi yapata nyongeza ya bajeti mwaka wa fedha 2019/2020

    (GMT+08:00) 2019-03-25 19:19:16
    Sekta ya uchukuzi nchini Tanzania imepata ongezeko la bajeti kutoka Sh2.39 trilioni katika mwaka wa fedha 2018/2019 hadi Sh3.62 trilioni mwaka wa fedha 2019/2020.

    Hayo yalisemwa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dk Leonard Chamuriho katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Sekta ya Uchukuzi ambao ulilenga kupitia na kupitisha Bajeti ya Sekta ya Uchukuzi fungu namba 62.

    Chamuriho alisema bajeti hiyo itatumika kutekeleza miradi mingi mikubwa itakayokuwa inaendelea kama vile mradi wa reli ya kisasa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro.

    Aidha alisema mradi mwingine ambao utafadhiliwa na fedha hizo ni ujenzi wa reli hiyo kipande cha Morogoro hadi Makutupora chenye urefu wa kilomita 422.

    Aidha alisema wanaendelea kuimarisha shirika la ndege Tanzania (ATCL) na wataendelea kukamilisha mipango iliyopangwa awali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako