• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yavutia uwekezaji wenye gharama ya $7.5bn katika miaka mitano iliyopita

    (GMT+08:00) 2019-03-25 19:19:46
    Uganda imetoa leseni kwa miradi 1,900 yenye gharama ya $7.5b katika mipango ya uwekezaji katika miaka mitano.

    Kulingana na takwimu kutoka Mamlaka ya Uwekezaji ya Uganda (UIA),nchi hiyo imevutia miradi 1,900 dhidi ya malengo ya miradi 1,500 katika sekta tofauti za uchumi tangu mwaka 2013.

    Katika mwaka wa fedha 2013/14,UIA ilitoa leseni kwa miradi 461 yenye gharama ya $2b, ambayo ilipungua katika mwaka wa fedha wa 2014/15 hadi $1.4b kutoka kutoka miradi 327.

    Katika mwaka wa fedha 2015/2016 UIA ilipata $1.5b kutoka miradi 353 ,ambayo iliongezeka hadi miradi 512 mwaka 2016 yenye gharama ya $1.6b.

    Ikiwa na malengo ya miradi 300,UIA ilitoa wastani wa leseni 350 za miradi isipokuwa mwaka 2017.

    Mwaka 2017 uliandikishwa kama mwaka mbaya kwa sekta ya uwekezaji ambapo miradi 247 yenye gharama ya $876m ilipatiwa leseni,ikiwa ni punguzo la asilimia 47 kutoka mwaka 2016.

    Kulingana na UIA ,anguko hilo lilisababishwa na kipindi cha mpito cha wawekezaji hadi mfumo wa utoaji leseni wa kielektroniki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako