• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Droo ya AFCON 2019 kufanyika April 12 mwaka huu

    (GMT+08:00) 2019-03-26 08:52:14
    Droo ya upangaji wa makundi ya fainali za (AFCON 2019) inatarajiwa kufanyika Aprili 12 mwaka huu nchini Misri ambapo Tanzania na Kenya zimewekwa kwenye chungu cha nne ikiwa pamoja na mataifa ya Mauritania, Namibia, Benin na Madagascar.

    Wenyeji Misri wako katika chungu cha kwanza pamoja na timu zilizojuu katika viwango vya ubora wa soka barani Afrika, ikiwa na Cameroon, Ghana, Ivory Coast, Tunisia na Senegal.

    Chungu cha pili kina timu za Morocco, Nigeria, Algeria, Guinea, Mali na DRC. Huku chungu cha tatu kinahusisha timu za Uganda, Afika Kusini, Guinea Bissau, Zimbabwe, Angola na Burundi.

    Vyungu hivyo vimepangwa kwa mujibu wa viwango vya soka vya CAF, ambapo makundi sita yanatarajiwa kuundwa, kila kundi likiwa na timu nne na timu zilizo kwenye chungu kimoja hazitakutana kwenye kundi moja.

    Hii ni mara ya kwanza kwa Afrika Mashariki kuingiza timu tano kwa wakati mmoja kwenye michuano hiyo, ambazo ni Burundi, DRC, Kenya, Tanzania na Uganda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako