• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa zamani wa Brazil Temer aachiwa huru kutoka gerezani

    (GMT+08:00) 2019-03-26 09:00:39

    Rais wa zamani wa Brazil Michel Temer na wasaidizi wake muhimu saba wameachiwa huru kutoka gerezani kufuatia kukamatwa kwao wiki iliyopita kwa makosa ya ufisadi. Bw. Temer aliachiwa huru na jaji Antonio Athie siku mbili kabla ya jopo la majaji kutarajiwa kutoa uamuzi kuhusu ombi lililotolewa na timu ya utetezi ya Bw. Temer. Bw. Athie amesema baada ya kupitia kesi hiyo kwa makini, amethibitisha kuwa hakuna sababu halali ya kusubiri siku nyingine mbili kuhusu kuachiwa huru. Ameongeza kuwa kwa mujibu wa Katiba, mtuhumiwa ana haki ya kuwa huru anaposubiri kesi yake kufunguliwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako