• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais Xi na Macron wakubaliana kuhimiza uhusiano imara kati ya nchi zao

    (GMT+08:00) 2019-03-26 09:14:54

    Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron, jana kwenye kasri la Elysee walikubaliana kuhimiza uhusiano wa ngazi ya juu kati ya nchi zao uwe imara zaidi, na kufanya ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili ufikie katika mwanzo mpya wa kihistoria.

    Rais Xi amesema mabadiliko makubwa yametokea kwenye hali ya kimataifa, lakini uhusiano kati ya China na Ufaransa mara zote umekuwa ukiendelea katika hali ya juu na imara. Amesema tangu Rais Macron alipoingia madarakani, katika chini ya muda wa miaka mwili uhusiano kati ya pande mbili umepiga hatua kubwa.

    Rais Xi pia ametaja kuwa huu ni mwaka wa maadhimisho ya kipekee, kwani kuna maadhimisho ya miaka 55 ya uhusiano kati ya China na Ufaransa, miaka 100 ya Harakati ya vijana wa China kwenda kusoma nchini Ufaransa, na miaka 70 ya maadhimisho ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya watu wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako