• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo nje wa China atoa mapendekezo ya kutaka kuwepo kwa usimamizi bora wa dunia

    (GMT+08:00) 2019-03-26 09:15:19

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana kwenye sherehe ya ufunguzi wa kongamano la usimamizi wa dunia mjini Paris, ametoa mapendekezo matatu ya kutafuta suluhisho la usimamizi wa dunia ambao ni wa haki zaidi, wenye ufanisi zaidi na unaoendana na mikondo ya historia.

    Bw. Wang ambaye ameambatana na Rais Xi kwenye ziara yake barani Ulaya, amesema jumuiya ya kimataifa inataka kuziona China na Ufaransa, zinafanya juhudi kwa pamoja kuhimiza maendeleo na amani ya dunia, wakati dunia inakabiliwa na matatizo.

    Waziri Wang amesema dunia ya sasa ina fursa na changamoto, na kusema uhusiano kati ya China na Ufaransa uko karibu sana na mawasiliano kati ya watu yamekuwa rahisi zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako